Michezo

Ajax yashikilia matumaini ya kusajili kipa wa Arsenal licha ya ofa ya awali kukataliwa


KLABU ya Amsterdam Ajax imewasilisha maombi ya kumnunua kipa Aaron Ramsdale wa Arsenal licha ya ofa yao ya awali kukataliwa.

Akiondoka, Arsenal itabakia na David Raya aliyerejea klabuni akitokea Brentford alikocheza kwa mkopo.

Tayari The Gunners imeripotiwa kuwa katika mazungumzo na Joan Garcia wa Espanyol ya Uhispania awe msaidizi wa Raya.

Ramsdale anataka kuagana na Arsenal ili ajiunge na timu ambayo itamhakikishia nafasi katika kikosi cha kwanza msimu huu wa 2024/2025 ulioanza majuzi.

Tangu Arsenal imnunue Raya, Ramsdale aliye na umri wa miaka 26,  amewahi kuwepo kwenye kikosi cha kwanza katika mechi 11 pekee katika mashindano tofauti msimu uliopita.

Iwapo Ajax itafaulu kumtwaa mlinda lango huyo, Ramsdale ataungana na kiungo wa zamani wa Liverpool, Jordan Henderson katika klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Uholanzi.