Ajenti wa Bale achemkia mashabiki wa Real madrid kwa kudharau mteja wake

Ajenti wa Bale achemkia mashabiki wa Real madrid kwa kudharau mteja wake

Na MASHIRIKA

AJENTI wa Gareth Bale, Jonathan Barnet, amekashifu mashabiki wa Real Madrid kwa kumkejeli staa huyo.Barnet amesema hajali kile ambacho mashabiki wamekuwa wakifikiria kuhusu Bale, ila wanafaa wamheshimu kwa kuwa aling’aa akisakatia timu hiyo siku za ubora wake.

Hivi majuzi, baadhi ya mashabiki wa Real walimtusi na kumzomea Bale karibu na uga wa mazoezi wa timu hiyo, Valdebebas.Barnett pia alisema hana uhakika kuwa winga huyo atasalia Real msimu ujao, kutokana na kejeli hizo. Kandarasi ya nyota huyo inakamilika msimu wa 2022/23.

mashabiki wa vigogo hao wa Uhispania. Kandarasi na Real Madrid inakamilika msimu wa 2022/23Bale ambaye pia amewahi kuchezea Tottenham Hot Spurs anauguza jeraha na amechezea Madrid mechi tatu pekee msimu huu. Mechi hizo zilikuwa dhidi ya Alaves, Levante na Real Betis.

You can share this post!

Mabwanyenye wapya Newcastle nao pia wajishasha kuwania...

Ni kisasi tu wikendi hii!

T L