Kimataifa

Ajikata nyeti na kuzihifadhi kwa jokofu

May 26th, 2019 1 min read

MASHIRIKA Na PETER MBURU

MWANAMUME mmoja nchini Marekani alitumia kisu kukata nyeti zake zote, katika juhudi za kujikomboa kutoka minyororo ya kuwa katika jinsia yoyote, kisha akahifadhi viungo hivyo katika jokofu.

Trent Gates mwenye umri wa miaka 23 kutoka Washington DC alijikata sehemu hizo katika utaratibu wa kisayansi aliofanyia nyumbani kwake Aprili 2016.

Gates alisema kuwa alitumia matembe ya kupunguza uchungu pekee, akisema kuwa kilichompa motisha ni hali kuwa akiwa na umri wa miaka 15 alimuona mtu mwingine aliyekuwa hana jinsia, kwa jina Gelding.

Baada ya kujikata na kubaki si mwanamume wala si mwanamke, hali yake sasa huko US inafahamika kama ‘Nullo’ ama ‘Smoothie’, kwa maana ya mtu ambaye amefanyiwa upasuaji ama uchunjaji kuondoa sehemu zinazomfanya kuwa wa jinsia fulani.

‘Nilitumia kisu aina ya ceramic kwa kuwa kinakata vyema na kwa utaratibu,” akasema Gates, ambaye ni mtaalam wa kiteknolojia.

Alisema baada ya kujikata, alienda hospitalini ili kuhakikisha kuwa kila kitu kilikuwa sawa kimatibabu.

Gates alisema ili kuendelea kwenda haja ndogo bila matatizo, aliacha kijishimo palipokuwa uume, akiongeza kuwa alihisi furaha tele alipofanikiwa kujifanyia hivyo.

Alisema furaha yake ni hisia anayopata kwa kufahamu kuwa sasa yeye si mwanamume wala mwanamke, ila yuko katikati tu.

Gelding, ambaye Gates alifurahishwa na hali yake, alijikata nyeti mnamo 2000, kisha akajikata uume 2011.

Akizungumza kuhusu hisia zake baada ya kujifanyia hivyo, Gates alisema “Nina furaha, najihisi kuwa mimi mwenyewe, najihisi nimepata uhuru zaidi.”