Habari Mseto

Ajipata taabani kwa kuiba vipuri vya gari la Jaji Mkuu David Maraga

April 17th, 2020 1 min read

NA RICHARD MUNGUTI

Waliosema mchovya asali hachovyi mara moja hawakukosea kwani mshukiwa wa vipuri vya magari ya Serikali alijipata taabani Alhamisi asubuhi.

Hakimu mwandamizi Martha Nanzushi Alhamisi aliamuru polisi wamtie nguvuni Juma Rama anayedaiwa aliiba vipuri kutoka kwa gari la Jaji mkuu David Maraga aliye pia rais wa Mahakana ya Juu nchini Kenya.

Huku akidhania maafisa wa usalama walikuwa wamelala baada ya kushika doria za kafyu usiku kucha alikuta sivyo.

Rama mwenye umri wa miaka 21 alijidanganya kuwa hakuna walinzi na maafisa wa polisi katika Mahakama ya Juu kufuatia agizo korti zifungwe kuzuia kuenezwa kwa gonjwa la corona linalokera na kusumbua wanadamu kote ulimwenguni.

Kutokana na dhana hiyo potovu Rama alinyapanyapa na kuingia katika egesho la magari ya majaji wa Mahakama ya Juu na Mahakama ya Rufaa katika barabara ya City Hall jijini Nairobi

Hii ilikuwa mara ya pili kwa Rama kuvamia egesho la magari ya Serikali. Mara ya kwanza ilikuwa Aprili 7 2020.

Aliingia katika Wizara ya Elimu na kung’oa vifuniko vya gari la wizara hiyo ya Elimu vyenye thamani ya Sh30,000.

hivyo vya gari rasmi la Jaji Maraga nambari ya usajili GKA 347F. Picha/ Richard Munguti

Mnamo Aprili 9 Rama alipiga moyo konde na kuingia katika egesho la Mahakama ya Juu na kunyemelea gari rasmi la Jaji Mkuu David Maraga na kuiba vifuniko vya mataa zenye thamani ya Sh20000.

Rama aliyeshtakiwa mwanzo mbele ya hakinu mwandamizi Bernard Ochoi alishtakiwa kunyofoa vifuniko

Kabla ya kuulizwa ajibu mashtaka matatu, Rama  aliomba mahakama iamuru apelekwe hospitali akidai alichapwa kama mbwa na kuumizwa.

Hakimu mwandamizi Martha Nanzushi . Picha/ Richard Munguti

“Mheshimiwa naomba uamuru nipelekwe hospitali. Nilipata kichapo cha mbwa kutoka kwa maafisa wa polisi walionishika katika mahakama ya juu,”Rama.

Aliongeza kusema: ” Nilivumaniwa punde nilipong’oa vifuniko hivyo. Nilipigwa jama mbwa.Nimeumizwa kabisa.”