Kimataifa

Ajipiga risasi akijaribu kuua kombamwiko

March 21st, 2019 1 min read

MASHIRIKA Na PETER MBURU

MWANAMUME kutoka Michigan, Marekani alijipiga risasi mguuni wakati alipokuwa akitupa kiatu baada ya kugundua kuwa kilikuwa na Kombamwiko.

Kulingana na maafisa wa serikali eneo hilo, mwanamume huyo kutoka mtaa wa Detroit mwenye umri wa miaka 50anasemekana kuwa alimwona mdudu huyo akivuka chumbani Jumanne, ndipo akaamua kumuua.

Kwa kuwa yeye ni kiwete, alichukua kiatu na kumrushia ili kumgonga, akisahau kuwa kulikuwa na bastola ndani ya kiatu, huku wakati tu kilipoanguka, bastola hiyo ilianguka nje na kutoa risasi ambayo ilimpata mwanamume huyo mguuni.

Hata hivyo, hakuumia sana kwani alikimbizwa hospitalini na akatibiwa, japo haijafahamika ikiwa alifanikiwa kumgonga kombamwiko huyo.