Habari Mseto

Ajiua akisubiri matokeo ya corona

August 1st, 2020 1 min read

NA FAUSTINE NGILA
Mwanaume mmojsa kutoka kaunti ndogo ya Rongai kaunti ya Nakuru alijitia kitanzi Jumamosi alipokuwa akisubiri matokeo yake ya virusi vya corona.

Maafisaa wa afya wa kaunti walisema kwamba mwanaume huyo amabye alikuwa  wa miak hamsini alijitia kitanzi kutumia pazia kwenye wadi ya kutenga watu ya hospitali ya War Memorial.

Alipatikana amefariki na dakatri aliyekkuwa na akifanya ukakuzi wa kawaida.

Mwanaume huyo alilazwa hospitalini baada ya kuonyesh adalili za virusi vya corona.

“Alikuewa na dalili za kukohoa ,shida ya kupumua,joto jingi mwilini..Alijiua kabla ya matokeo yake kutoka ,” afisa mkuu wa wa afya Dkt Samuel King’ori aliambia Taifa Leo.

Dkt King’ori alisema kwamba mwanaume huyo alisafiri kutoka Nairobi wakati Rais Uhuru Kenyatta alifungua safari za kutoka Nairobi,Mombassa na Manddera July 6.

“Alijiunga nafamilia yake Rongai na akaenda hospitali baada ya kupata dalili za corona.Alifanyiwa kipimo cha corona na akawekwa karantini,”alisema.

Matokeo ya vipimo yalionyesha kwamba mwanaume huyo alikuwa na virusi vya corona.

Mwili ulipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhi mahiti cha hospitali hio na mazishi kuwekwa Jumapili.

Nakuru imerekodi visa 234 vya corona vikipungua.