Habari Mseto

Ajiua baada ya kumjeruhi mkewe

October 28th, 2020 1 min read

NA BRIAN OJAMAA

Wingu al huzuni limetanda Kijiji cha Namarambi Wadi ya Ndivisi eneobunge la Webuye Mashariki Kaunti ya Bungoma baada ya mwanamme kujitia kitanzi baada ya mzozo na mkewe.

Maurice Natembeya alijitia kitanzi baada ya kumvamia na kumuumiza mkewe.

Nduguye Bw Martin Kapilo alisema kwamba familia bado haikuamini kitendo alichotenda nduguye

Alisema kwamba wawili hao wamekuwa na matatizo ya ndoa na kwamba nduguye alimvamia na kumuumiza mkewe mwaka jana huku akimuacha majeraha mabaya.

Kufuati kisa hicho kilichotokea Juni mwaka jana mwendazake alijificha kwa shamba la miwa ili asikamatwe.

“Nimekuwa nikimuonya dunguyangu kuhusina na maswala ya vita na vurugu.Ona sasa alichofanya ni aibu kubwa.Mkewe nauguza majeraha kwenye hospitali ya kaunti ya Webuye ,” alisema nduguye.

Daktari Simon Kisaka alisema kwamba mwanamke huyo alipata majeraha ya kichwani, shingoni na mgongoni.

Tafsiri na Faustine Ngila