Ajiua sababu ya mke kuwa na mpango wa kando

Ajiua sababu ya mke kuwa na mpango wa kando

Na KALUME KAZUNGU

MWANAMUME wa makamo (pichani) Jumanne alijitia kitanzi baada ya kugundua kuwa mkewe alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamume mwingine.

Mwili wa Philip Ngugi,30, ulipatikana ukining’inia kwenye mti karibu na nyumba yake katika kijiji cha Matanya, tarafa ya Mpeketoni, Kaunti ya Lamu.

Afisa Mkuu wa Polisi (OCPD) wa eneo la Mpeketoni, Christopher Limo, alisema: “Ni kweli. Kuna mwanamume ambaye amejitia kitanzi asubuhi ya leo. Polisi tayari wamefika kwenye eneo la tukio. Tunashuku tukio hilo limechangiwa na mzozo wa kimapenzi. Tunachunguza na ikiwa kuna yeyote amehusika tutamkamata na kumhoji ili kubaini sababu zilizopelekea jamaa huyo kujitoa uhai.”

Baadhi ya wanakijiji waliozungumza na Taifa Leo walisema mwendazake alikuwa ameteketeza nyumba yake miezi miwili iliyopita kabla ya kwenda mafichoni.

Mwili ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ndogo ya kaunti mjini Mpeketoni.

You can share this post!

Msaidizi wa gavana ndani kwa kuteka nyara mwanahabari wa NMG

UGAIDI: Al Shabaab walazimisha wakazi kukosa huduma muhimu

adminleo