Mlofa mwizi ajuta baada ya simu kuita jina la mwenyewe

Mlofa mwizi ajuta baada ya simu kuita jina la mwenyewe

Na DOMINIC MAGARA

KISAUNI, MOMBASA

KALAMENI anajuta kuiba simu ya mkono sokoni ilipoanza kuita jina lake alipoifungua.

Kioja kilizuka punde tu jamaa alipofika nyumbani na kutaka kutoa laini ya mwenye simu aweke yake.

“Mbona wanifungua? Wataka kuniuza, utajua hujui, nirudishe ulikonitoa haraka.” Jamaa alipuuza sauti hiyo na kuendelea kuichokora.

Mara simu ilianza kuwa kubwa na kubadilika kuwa paka!

Aliruka juu na kukumbuka vituko vya paka kutaja majina ya watu na kuwasalimia huku wakati mwingine wakicheka kama binadamu.

Majirani walimsikia akiomba simu msamaha kwa sauti ya juu sana.

Alichomoka nje ya nyumba huku akilia.

Aliwaeleza makosa yake ya kuibia ajuza simu yake ya mkono. Sauti ya paka ilisikika ikiitikia.

Aliondoka mbio na kuirudisha ikiwa salama kuokoa maisha yake.

  • Tags

You can share this post!

Nyumba ya gaidi wa Al Shabaab kutwaliwa na serikali

WANDERI KAMAU: Mataifa yaungane kukabili Omicron, sio...

T L