Dondoo

Akaidi mama yake na kuoa kiosha roho wake

Na LEAH MAKENA September 2nd, 2024 1 min read

TAYARI, MOLO

MAMA wa hapa aliambulia patupu kidosho aliyekuwa akichukia alipofunga pingu za maisha na mwana wake. Inasemakana kuwa kidosho alipofikishwa kwa mama ili atambulishwe, alimkataa akisema hakuwa na maadili mema.

“Wachana na huyu kiruka njia wa mjini, nitakutafutia mrembo mwenye heshima,” mama alisema.

Habari zasema kuwa kampeni za mama za kufanya kidosho atemwe ziliambulia patupu kwani kijana wake alifanya harusi ya kukata kata na shoka na hatimaye kuonya mama yake dhidi ya kuingilia ndoa yake.