Akamatwa baada ya kuua mkewe na watoto wake wawili

Akamatwa baada ya kuua mkewe na watoto wake wawili

Na BENSON MATHEKA

Maafisa wa Uchunguzi wa Uhalifu (DCI) Kaunti ya Embu wanachunguza kisa ambapo mwanamume anashukiwa kumuua mkewe mwenye umri wa miaka 28 na watoto wao wawili wa umri wa miaka tisa na mitano.

Kwenye taarifa kupitia Twitter, DCI ilisema kwamba kisa hicho kilitendeka alfajiri Jumapili. Idara hiyo ilisema kwamba mshukiwa aliyetambuliwa kwa jina David Kariuki Nyaga alifungia famila yake ndani ya nyumba yao iliyoko kijiji cha Kiamukuyu, kabla ya kuwaua mmoja baada ya mwingine.

Maafisa hao walitaja mauaji hayo kama ya kutisha mno. DCI ilisema maafisa wake walikuwa wamefahamishwa kuhusu kisa hicho na naibu chifu wa eneo hilo Anthony Munyiri lakini walipofika nyumbani kwa mshukiwa walipata alikuwa ametekeleza mauaji kwa kutumia nyundo kuwapinga utosini.

“Silaha hiyo ilipatikana na mshukiwa akatiwa mbaroni huku wapelelezi wakijaribu kubaini kilichomfanya kutekeleza mauaji hayo,” ilisema taarifa ya DCI. Mshukiwa atafikishwa kortini kujibu mashtaka ya mauaji.

You can share this post!

MIIBA TELE MBELE YA UHURU

Muuguzi asimulia alivyolazimishwa kupashwa tohara akiwa na...