Kimataifa

Akamatwa kwa kufanya ngono na mbwa 158 na paka 17

May 15th, 2019 1 min read

MASHIRIKA Na PETER MBURU
 
MFANYAKAZI wa shirika la kuwatunza mifugo alikamatwa wiki hii, akidaiwa kuwa amewadhulumu kingono mbwa 158 na paka 17 kwa muda wa miaka miwili.
 
Barney Clifton ambaye ana miaka 51 alikamatwa na polisi wa idara ya Detroit, akikumbana na jumla ya mashtaka 1561, yakiwemo kushiriki ngono na wanyama na kudhulumu wanyama.
 
Polisi wanasema Clifton kwa miaka miwili amefanya ngono na mbwa 158 na paka 17, mbali na kurekodi picha za ngono akijisifu kuwa daktari wa kutibu hali ya wanaume wenye uume mdogo.
 
Polisi aidha walisema kilichowafanya kugundua kuwa mshukiwa ndiye aliyekuwa akiwadhulumu wanyama hao ni hali kuwa alikuwa na tabia ya kuwawinda na kuwakamata mbwa.
 
Vilevile, mwanamume huyo anakumbana na mashtaka ya kurekodi na kuchapisha mitandaoni picha za ngono. Polisi wamesema kuwa bado wanafikiria kumuongezea mashtaka mengine kadri uchunguzi unavyoendelea kufanywa.
 
Mwanamume huyo, hata hivyo, anadaiwa kuwa hana akili timamu kwani amewahi kukaa katika hospitali ya wenda wazimu kwa miaka mitano. Wakili wake Robert Fitgerald ametangaza ataiomba korti kumtaka afanyiwe ukaguzi wa kiakili.