Akamatwa kwa kumfanyia mpenziwe mtihani

Akamatwa kwa kumfanyia mpenziwe mtihani

Na AFP

MWANAFUNZI nchini Senegal amekamatwa na kuzuiliwa na polisi kwa madai ya kumsaidia mpenziwe kufanya mtihani wa shule ya upili.

Kulingana na polisi jana, mwanamume huyo alijifanya mwanamke ili kutotambulika kwa urahisi na wasimamizi wakuu wa shule hiyo.

Mpenziwe pia amekamatwa.Kulingana na wakili wa mshukiwa huyo, Serigne Ndiongue, wapenzi hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani leo.

Watafunguliwa mashtaka ya kupanga njama ya kufanya udanganyifu.“Wamefunguliwa mashtaka ya udanganyifu na walalamishi. Hata hivyo, tuko tayari kuwatetea wateja wetu kuonyesha wanasingiziwa kufanya makosa hayo bila sababu wala ushahidi wowote,” akasema wakili huyo.

Wawili hao wamekana madai hayo.Kijana huyo, ambaye yuko katika chuo kikuu, alisafiri hadi katika mji wa Diourbel ili kufanya mtihani huo kwa niaba ya mpenziwe.

 

You can share this post!

CHARLES WASONGA: Tukatae mswada wa kulipia wabunge bima ya...

Vita vikali Afghanstan huku zaidi ya watu 40 wakiuawa