Habari Mseto

Akana kudukua akaunti za benki na kuiba Sh12 milioni

April 2nd, 2019 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

MSHUKIWA wa udukuzi wa akaunti za benki alishtakiwa Jumanne kwa kufanya njama za kuibia benki ya Chase zaidi ya Sh12 milioni.

Edwin Cheloti Wanyama alishtakiwa mbele ya hakimu mkuu mahakama ya Nairobi Bw Francis Andayi.

Alikanusha mashtaka mawili ya kufanya njama za kudukua akaunti za benki hiyo na kuiba Sh12,504,000 kati ya Juni 7 na Julai 8 2018.

Shtaka lilisema alifanya njama hizo akishirikiana washukiwa wengine ambao wameshtakiwa.

Kesi dhidi yao itaunganishwa na nyingine.

Aliachiliwa kwa dhamana ya Sh500,000 hadi Julai 3 kesi itakaposikizwa.