Habari Mseto

Akana shtaka la wizi akisema 'niliiba kujikimu kimaisha'

August 8th, 2018 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

MUUZAJI katika maduka yaliyo kwenye jengo la kibiashara la Jamia Mosque, Nairobi Jumanne alikanusha kuiba mishipi mitatu yenye thamani ya Sh3,000.

Bi Amina Hussein Mohammed (kushoto mwenye hijabu ya rangi ya zambarau) alikana aliiba mishipi hiyo ya mwajiri wake Bw Mohammed Mohamud mnamo Julai 16.

Akiomba aachiliwe kwa dhamana, Bi Amina alisema “aliiba kujikimu kimaisha.”

Mshtakiwa alimsihi hakimu amwonee huruma kwa vile maisha ni magumu na “alichukua mishipi hiyo kuiuza kujisaidia.”

Mahakama iliamwamuru alipe dhamana ya pesa tasilimu Sh3,000.

Kesi itasikizwa Agosti 20, 2018.

Upande wa mashtaka uliamriwa umkabidhi mshtakiwa nakala za mashahidi.