Habari Mseto

Akatwa kwa panga na mwanajeshi akiiba kuku

October 13th, 2020 1 min read

NA CHARLES WANYORO

Mwanamume wa miaka 23 anauguza majeraha baada ya kuchomwa na panga na mwanajeshi mmoja kwa madai kwamba aliiba kuku wake kijiji  cha Kagwani Igoji Mashariki, Kaunti ya Meru.

Bw Dennis Kinyua anauguza majeraha kwenye hospitali ya Kanyakine baada ya mashambulizi hayo ya usiku.

Alisema kwamba mwanajeshi huyo aliyetambulika kama Danson Mutuma Kithinji anayeishi Kahawa Garrison alimvamia usikualipokuwa akilala  siku 12 zilizopita.

Wapelelezi kutoka kitego cha vita pamoja na polisi walitembelea mgonjwa huyo Jumanne na baadaye wakamkamata Mutuma.

Mkuu wa polisi wa Imenti Kusini William  Maronga alisema kwamba alikuwa katika mazungumzo na mwanajeshi huyo na walikuwa wampeleke kortini.