Akida arejea Starlets, Alumirah akitaja kikosi cha muda

Akida arejea Starlets, Alumirah akitaja kikosi cha muda

NA RUTH AREGE

MVAMIZI wa Harambee Starlets Essie Akida ni kati ya nyota ambao Jumanne waliunga kikosi cha muda kilichotajwa kwa mechi ya raundi ya pili ya kufuzu kipute cha Mataifa Bingwa Afrika kwa Akina Dada (AWCON).

Kocha mpya Alex Alumirah jana alimjumuisha Akida ambaye alichezea Starlets miaka miwili iliyopita na sasa anaisakatia FC POAK Thessaloniki ya Ugiriki .

Nyota huyo wa zamani amekuwa akiachwa nje na waliokuwa wakufunzi wa Starlets David Ouma (sasa Naibu wa Kocha wa Sofapaka) na mtangulizi wa Alumirah, Charles Okere japo alikuwa akiridhishwa kila mara alipojumuishwa kikosini.

Aidha baadhi ya nyota ambao walijumuishwa katika kikosi hicho ni aliyekuwa mnyakaji wa Vihiga Queens Lillian Awuor na mshambuliaji Jentrix Shikangwa, wote waliohama timu hiyo wiki jana.

Awuor alijiunga na Soyaux ya Ufaransa huku Shikangwa akisakatia Fatih Karagumruk Sportif ya Uturuki.

Katika orodha hiyo Vihiga inaongoza kwa wachezaji wanane huku mabingwa watetezi wa WPL Thika Queens wakiwakilishwa na wachezaji watano.

Ulinzi Starlets, Wadadia na Mathare Women wana mchezaji mmoja kila moja kikosini.

Starlets kucheza na Crested Cranes ya Uganda jijini Kampala Februari 16 kabla ya kuwaandaa nchini siku saba baadaye ( Februari 23).Kenya ilifuzu kuingia raundi ya pili ya mchujo baada ya kuifunga Sudan Kusini jumla 15-1 ugani Nyayo Oktoba, 2021.

Awcon itafanyika Morocco kuanzia Julai 2-Julai 23 na timu tano zinatarajiwa kufuzu kuwakilisha Afrika katika Kombe la Dunia litakaloandaliwa Australia na New Zealand mwakani.

Mara ya mwisho kwa Kenya kushiriki Awcon ni mnamo 2016 kule Cameroon ila ikakosa makala ya 2018.

MAKIPA: Annette Kundu(AEL-Cyprus); Pauline Kathuru (Gaspo Women -KWPL); Lilian Awuor (Soyaux- France); Samantha Akinyi(Tigers Fc – Tanzania); Carolyne Rufa (Fountain Gate – Tanzania)

WALINZI: Leah Andiema(GASPO-KWPL); Vivian Nasaka (Vihiga Queens -KWPL); Juliet Andibo (Thika Queens -KWPL); Dorcas Shikobe (Lakatama FC-KWPL); Cyprus), Lucy Akoth (Ulinzi -KWPL); Phoebe Owiti (Vihiga Queens -KWPL); Enez Mango (Vihiga Queens-KWPL); Wincate Kaari (Thika Queens-KWPL)

KIUNGO: Sheril Angachi (Ulinzi Starlets-KWPL); Corazone Aquino (Gaspo Women-KWPL); Mercy Oginga (Vihiga Queens-KWPL); Lydia Akoth(Thika Queens-KWPL)

MASTRAIKA: Terry Engesha (Vihiga Queens-KWPL); Jentrix Shikangwa (Fatih Karagumruk- Turkey); Mwanalima Adam Dogo (Hakkaragicu-Turkey); Violet Wanyonyi (Trans Nzoia-KWPL)Essie Akida (PAOK-Greece) Mercy Airo (GASPO-KWPL)Elizabeth Wambui (Gaspo -KWPL)

  • Tags

You can share this post!

Uhuru ajibu mishale ya Ruto Magharibi

Bandari yajiandalia Tusker, mastaa wanne kukosa mechi

T L