AKILIMALI: Ni miaka 40 sasa akishona nyavu za samaki, kazi inayomsomeshea wanawe hadi chuoni

AKILIMALI: Ni miaka 40 sasa akishona nyavu za samaki, kazi inayomsomeshea wanawe hadi chuoni

Na WINNIE ONYANDO

KUFANIKIWA katika kila jambo ni sharti ujitoe mhanga na uwe mvumilivu.

Katika mtaa wa Uyawi kwenye ufuo wa Ziwa Victoria, Kaunti ya Siaya, Mzee Joel Onyando, 63, anatueleza safari yake ndefu ya kushona nyavu za uvuvi.

Ziwa hilo ni kitovu cha uvuvi na huwa na spishi mbalimbali za samaki wenye ladha ya kipekee; hutochanganywa kiladha na wale samaki wa ‘China’.

Ili kuwanasa vyema ni sharti mvuvi awe na wavu mzuri kufanikisha kazi yake. Hapa ndipo Mzee Joel hupata umaarufu.

Anaeleza kuwa changamoto tele zilizowakumba wakiwa wachanga, hasa kufuatia kifo cha babake 1990, ndizo zilimsukuma kujitosa katika ushonaji nyavu kama kitega uchumi.

Hii ni baada yake kuacha shule mnamo 1974 akiwa na umri wa miaka 18.

Baba huyu wa watoto 10 anasema amefanya kazi hiyo kwa zaidi ya miaka 40, ikimwezesha kusomesha watoto wake.

“Kupitia biashara hii wanangu wawili wamesoma hadi chuo kikuu, na wawili wamemaliza kozi katika chuo cha taasisi hapa. Wanne wako shule za upili, wote nawasomesha kupitia ushonaji wa nyavu za uvuvi,” aliambia Akilimali.

Amejenga kijumba anachotumia kushona na kuhifadhi nyavu za wateja.

Kama ilivyo ada kwa kitega uchumi chochote kile, kazi yake haijakuwa rahisi.

“Hesabu nyingi huhitajika katika kazi hii. Pengine mteja ameleta vifaa chache ila wewe kama mshonaji sharti utumie ujuzi wa kufanya hesabu kuhakikisha kuwa vifaa hivyo vinatosha bila kumuitisha vingine,” anaeleza.

Mzee Joel asema kuwa hajasomea kazi yake, ujuzi wa kushona ulimjia toka akiwa mdogo.

“Ningeshona sweta za nyuzi za kuchezea. Hapo ndipo niliamua kunoa ujuzi wa kushona nyavu za uvuvi,” anaeleza.

Wakazi wanaotoka eneo la Ziwa Victoria mara nyingi huwa wavuvi, lakini yeye hakukita katika shughuli hiyo na badala yake aliamua kuzamia biashara hii ya kushonea wateja nyavu.

Sababu shughuli kuu ya kiuchumi hapo ni uvuvi, alikuwa na soko tayari kwa bidhaa zake.

Vile vile, ustadi wake umevuka mipaka hadi kupata wateja nchini Uganda na Tanzania.

Yeye hushona nyavu kulingana na aina ya samaki watakaovuliwa.

“Tangu nianze kushona nyavu 1975 nimeunda zaidi ya 1,000. Mimi hushona kwa oda za wateja. Pia nyavu ikihitaji ukarabati, mimi ndiye fundi hodari,” Mzee Joel ajipigia debe.

Mambo kadhaa huzingatiwa na mvuvi kuamua aina ya nyavu atakazotumia. Rangi za kijani, bluu na kijivu ndizo huingiliana na maji, hivyo samaki hatafahamu ikiwa yupo majini au amenaswa.

Pili ni unene na umbo la tundu; ambapo za almasi, mraba na iliyo kingamana hubaini aina na saizi ya samaki watakaovuliwa.

Vifaa anavyotumia Mzee Joel kazini ni pamoja na kamba ya nailoni na sindano, ambazo hununua mjini Kisumu.

Hupata kati ya Sh20,000 na Sh50,000 kwa kila wavu kulingana na upana, ukubwa na gharama ya vifaa atakavyotumia.

“Kazi hii inataka uwe makini na chapuchapu kwani inaweza kukuchukua mwezi au miwili kushona wavu mmoja wa wastani.”

ubwa wa nyavu yenyewe.

, kifaa cha kuelea juu cha rangi mbalimbali (floats), Kamba au uzi aina ya nailoni ambayo imepindishwa (multifilament nylon net) na kitakachozamisha nyavu majini.

“Katika kushona nyavu moja nitasanya kila kitu nahitaji na kuanza kupiga hesabu idadi za kamba nitakazohitaji kushona nyavu yenyewe, nitachukua kalamu na kitabu na kuweka hesabu zangu chini. Hii ni kama uhandisi na unafaa kuwa na umilisi wa juu katika hisabati. Hesabu pia inahitajika katika kukadiri namna nyavu yenyewe itakavyokuwa,” alifafanua Joel.

Kila anachohitaji katika kufanikisha kazi yake Joel hununua katika duka la kuuza nyavu mjini Kisumu. Katika kushona nyavu moja mzee huyo hupata kati ya Sh20,000 na Sh50, 000 kulingana na upana, ukubwa na gharama ya vifaa atakavyotumia.

“Kwa kuwa kazi hii inahitaji umakini na uchapuchapu, nyavu moja huwa naweza kuchukua muda wa kati ya mwezi mmoja na mbili kulingana na hali ya anga na ukubwa wa nyavu yenyewe. Wakati wa baridi mimi hulemewa kufanya kazi kwa kuwa ninaugua ugonjwa wa kifua. Wakati wa jua mimi huanza kazi saa kumi na mbili asubuhi na kutamatisha saa kumi na mbili jioni,” Joel aeleza Akili Mali.

Kupitia hii kazi, mzee huyo ameweza kusafiri nchi ya Uganda na Tanzania ili kushonea wateja nyavu za uvuvi.

Kama kazi na biashara zingine, Joel anaeleza kuwa biashara yake ina changamoto nyini sana. Anaeleza kuwa wakati wa baridi yeye huugua na kulemewa na kushona nyavu za uvuvi. Wakati mwingine, wengine hawamlipi kwa wakati walioagizana.

“Nimeona chamgamoto nyingi sana, lazima nitafute pesa na kuwasomesha wanangu. Jua huwa kali wakati mwingine na siwezijisitiri kwa kuwa nyavu huwa ndefu na kuhitaji nafasi kubwa sana kushona. Wengine wanataka uwashonee kwa bei ya chini na hivyo kuwa changamoto kwangu,” alisema Joel.

Anawahimiza watu kujitia moyo kila mara kwa kuwa leo huenda ukakosa bali kesho ukabarikiwa na kufanikiwa.

You can share this post!

AKILIMALI: Alipoteza vyote katika ghasia za 1992 ila sasa...

KILIMO BIASHARA: Msomi wa biashara aliyezamia zaraa ya...