Habari Mseto

Akimbizwa spitalini baada ya kujikata nyeti

October 29th, 2020 1 min read

Vitalis Kimutai na Faustine Ngila

Mwanamume wa miaka 70 alikimbizwa hospitalini baada ya kujikata sehemu zake za siri kufuatia madai kwamba alikuwa na uhusiano nje ya ndoa.

Wakazi wa Kijiji cha Chep kochum eneo la Gatarwet eneobunge la Bureti walisema walishangazwa na tukio hilo.

Jamaa zake walisema kwamba walishuku kwamba alikuwa na mahusiano ya nje kwani alikuwa anatumia pesa nyingi kuliko zenye alikuwa akipokea kutoka kwa shamba lake la majani chai la hekari nne.

Walidai kwamba babu huyo alitumia pesa hizo kwa wanawake wengine na alikuwa ametekeleza familia yake.

Mwanamume huyo anasemekana kuwa amekodisha sehemu ya shamba lake na kutumia pesa hizo kujengea mwanamke mwingine wah apo kijijini nyumba.

“Alijifungia chumbani chake cha kulala na kukata sehemu zke za siri kwa kutumia kisu baada ya mkewe na wanawe kumkemea kuhusiana na mahusiano hayo,” alisema Bw Getarwet.

Ilisemekana kwamba mwanamume huyo alimkemea mkewe alipomuliza kuhusina na madai hayo na akaendela kutembelea wanawake wengine. Familia yake ilimpeleka kwenye hospitali ya AIC litein .