Habari Mseto

Al Shabaab wavamia basi la abiria

October 7th, 2020 1 min read

NA MANASE OTSIALO

Basi la abiria lilimiminiwa risasi na magaidi wa Al Shabaab  Mandera Kusini Jumanne huku Naibu kamanda wa polisi Joshua Kitakwa akisema kwamba majeruhi yaliripotiwa.

Kikundi hicho haramu kimekuwa kikiwavamia sehemu tofauti nchini tangu Kenya ijiunge na Amisom.

Mashambulizi mabaya yalifanyika kwenye chuo kikuu cha Garissa yaliyotokea Aprili 2,2015 ambapo watu 148 walifariki wengi wao wakiwa wanafunzi.

Mashambulizi mengine yalitokea kwenye jumba la Westgate Septemba 12,2013 huku watu 67 wakifariki kwenye tukio lililoendele kwa siku nne mfululizo..

Oktoba 6 watu watatu walitekwa nyara na Al shabaab kaunti ya Mandera. Wasafiri wanane walijeruhiwa wakati katika kisa cha hivi karibuni.

Bw Joshua Kitakwa alisema kwamba tukio hilo lilitokea mji wa Elwak na Kotulo.

“Bado hatujui idadi ya waliohumia kwa sasa lakini hakuna kifo kilochoripotiwa ,”alisema kupitia njia ya simu.

Ata hivyo  duru za kuaminika kutoka hospitali waliyopelekwa ya Kotulo zilisema kwamba watu wanne walikuwa kwenye hali mabya.

“Tumepokea waathiriwa wanane lakini wanne wako kwenye hali mabya,”zilisema habari hizo.

 

Tafsiri na Faustine Ngila