Habari Mseto

Aladwa aililia korti itamatishe kesi dhidi yake

June 19th, 2018 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

MBUNGE wa Makadara Bw George Aladwa Jumatano aliomba mahakama itamatishe kesi inayomkabili ya kueneza chuki akisema kuna uuwiano wa kitaifa sasa.

Akiwasilisha ombi hilo mbele ya hakimu mkuu Bw Francis Andayi, Bw Aladwa alisema baadhi ya kesi zilizokuwa zimewasilisha za jumbe za chuki zimeondolewa tangu Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa Nasa Bw Raila Odiinga wazindue ushirikiano.

“Naomba hii mahakama itatamatishe kesi dhidi ya Bw Aladwa kwa muktadha wa uhusiano uliozinduliwa miezi michache iliyopiita na Mabw Kenyatta na Odinga,” wakili Dkt John Khaminwa anayemwakilisha meya huyo wa zamani (aladwa) alisema.

Mbunge wa Makadara George Aladwa (kulia) akiwa na wakili wake Dkt John Khaminwa. Picha/ Richard Munguti

Dkt Khaminwa alisema uuwiano wa kitaifa umeendelea kuboroshwa na uhusiano mzuri baina ya Mabw Kenyatta na Odinga.

Dkt Khaminwa aliikabidhi korti nakala ya barua aliyoandikia tume ya utangamano na uuwiano wa kitaifa NCIC akiomba kesi dhidi ya Bw Aladwa itamatishwe.

Bw Aladwa anashtakiwa kwa kueneza chuki alipodai lazima watu wachache wafe endapo Bw Odinga hatatwaa hatamu za uongozi katika uchaguzi mkuu uliopita.

Dkt Khaminwa aliomba kesi dhidi ya Bw Aladwa itajwe Juali 12 wakati mmoja na kesi dhidi ya aliyekuwa Seneta wa Mackhakos ya uchochezi pia.

Mabw Aladwa na Muthama wamekanusha mashtaka ya kueneza chuki na uchochezi. Wako nje kwa dhamana.