Alaves wakomesha rekodi nzuri ya Atletico Madrid kwenye La Liga

Alaves wakomesha rekodi nzuri ya Atletico Madrid kwenye La Liga

Na MASHIRIKA

ATLETICO Madrid walipoteza nafasi maridhawa ya kutua kileleni mwa jedwali la Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga) baada ya Alaves kuwapepeta 1-0 katika kichapo ambacho kilikuwa cha kwanza kwa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu kupokezwa msimu huu wa 2021-22.

Hadi waliposhuka dimbani kumenyana na Atletico ya kocha Diego Simeone, Alaves walikuwa wamepoteza mechi zote tano za kwanza katika La Liga msimu huu.

Bao la pekee na la ushindi kwa Alaves lilifumwa wavuni na Victor Laguardia katika dakika ya nne baada ya kukamilisha kwa ustadi krosi ya Rodrigo de Paul.

Nusura Mamadou Loum afungie Alaves bao la pili katika dakika ya 60 ila kombora lake likadhibitiwa vilivyo na kipa Jan Oblak. Kati ya wanasoka wa Atletico waliojituma zaidi katika gozi hilo ni Angel Correa aliyemwajibisha vilivyo kipa Fernando Pacheco.

Matokeo hayo yanasaza Atletico na pointi mbili nyuma ya viongozi wa jedwali Real Madrid wanaotiwa makali na kocha Carlo Ancelotti.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Manchester City yalipiza kisasi dhidi ya Chelsea ligini

Mwanavoliboli Mkenya Chemos anyakuliwa na Mouloudia nchini...