Albania kichinjioni Uingereza leo Italia ikitifuana na Uswizi

Albania kichinjioni Uingereza leo Italia ikitifuana na Uswizi

LONDON, Uingereza

Na MASHIRIKA

Wenyeji Uingereza wanatarajiwa kuendelea kuvuma nyumbani watakapoalika Albania kwa mchuano muhimu wa kutafuta tiketi ya Kombe la Dunia 2022 dhidi ya Albania hii leo.

Uingereza hawajahi kupoteza nchini mwao katika mechi ya kufuzu kushiriki Kombe la Dunia tangu walimwe 1-0 na Ujerumani mwaka 2000.Mambo hayatarajiwi kuwa tofauti katika mechi hiyo ya Kundi I ugani Wembley ambayo viongozi Uingereza watajiweka pazuri kujikatia tiketi wakitia kibindoni alama tatu inavyotarajiwa.

Washambuliaji Harry Kane na Mason Mount walizamisha Albania 2-0 mwezi Machi ugenini. Kane bado ataongoza mashambulizi ya Uingereza akishirikiana na kinda matata Phil Foden naye mwanabunduki Emile Smith Rowe yumo mbioni kutumiwa na kocha Gareth Southgate kwa mara ya kwanza kabisa.

Southgate atakosa huduma za chipukizi matata Declan Rice, Marcus Rashford na Mount wanaoguza majeraha pamoja na wazoefu James Ward-Prowse na Luke Shaw.Albania, ambayo inakamata nafasi ya tatu kwa alama 15, inakaribisha Armando Broja kutoka mkekani na Endri Cekici aliyekosa mchuano uliopita dhidi ya Poland akitumikia marufuku ya kadi ya njano.

Mchuano mwingine wa kudondosha mate utakuwa kati ya viongozi wa Kundi C Italia na nambari mbili Uswisi. Timu hizi ziko bega kwa bega kwa alama 14 baada ya kuzoa ushindi mara nne na kuandikisha sare mbili.

Mshindi atajiweka pazuri kunyakua tiketi ya moja kwa moja kufika nchini Qatar mwaka 2022. Italia, ambayo ilikosa Kombe la Dunia 2018, itawategemea washambuliaji Federico Bernardeschi, Federico Chiesa na Lorenzo Insigne (pichani) na mabeki wazoefu Giorgio Chiellini na Leonardo Bonucci. Ciro Immobile na Lorenzo Pellegrini wako nje.

Granit Xhaka na Haris Seferovic ni majina makubwa yatakayokosa kwa upande wa Uswisi itakayotegemea Xherdan Shaqiri na Mario Gavranovic.

You can share this post!

Muujiza wa Conte kutoa maji kwenye mwamba pale Spurs

Villa yamwaga 674 Millioni kunyakua kocha Gerald

T L