Alexis Sanchez ayoyomea Ufaransa kuchezea Olympique Marseille baada ya kukatiza uhusiano na Inter Milan ya Italia

Alexis Sanchez ayoyomea Ufaransa kuchezea Olympique Marseille baada ya kukatiza uhusiano na Inter Milan ya Italia

Na MASHIRIKA
 
FOWADI wa zamani wa Arsenal, Manchester United na Barcelona, Alexis Sanchez, ametia saini mkataba wa miaka miwili na klabu ya Olympique Marseille nchini Ufaransa baada ya kuagana na Inter Milan ya Ligi Kuu ya Italia (Serie A).
 
Nyota huyo raia wa Chile aliyehudumu kambini mwa Arsenal kwa misimu minne, alifungia Inter mabao 20 kutokana na mechi 109 tangu aagane na Man-United mnamo 2019.
 
Sanchez, 33, aliongoza Inter kunyanyua taji lao la kwanza la Serie A baada ya miaka 11 mnamo 2020-21 licha ya kutokuwa tegemeo katika kikosi cha kwanza.
 
Inter wameratibiwa kufungua kampeni zao za Serie A mnamo 2022-23 dhidi ya Lecce mnamo Agosti 13, 2022.
 
TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO
  • Tags

You can share this post!

Usalama waimarishwa Mavoko kura zikihesabiwa

Jeremiah Kioni akubali kushindwa katika eneobunge la...

T L