Dondoo

Alipia kitanda alichovunja akimumunya uroda

August 27th, 2019 1 min read

NA NICHOLAS CHERUIYOT

KERICHO MJINI

ILIBIDI polo wa hapa kumnunulia rafiki yake kitanda kipya baada ya kuvunja chake akiramba asali ya kisura.

Udaku uliodunda katika meza ya dondoo unaarifu kuwa polo alimpata rafiki yake na kumrai amuachie chumba chake kwenye ploti ya mji huu alishane uroda na demu mmoja.

“Urafiki ni kufaana bwana. Nimefanikiwa kumtongoza kipusa na amenikubali. Uniachie chumba leo alasiri hii yote niwe na raha na binti huyo,” jamaa alimlilia mwenzake.

“Sitaki chumba changu kutumiwa kwa mambo ya ufuska. Mchumba wangu ni Mkristo na hapendi chumba changu kutiwa doa ya usherati,” rafiki ya polo alimjibu mwenzake.

Hata hivyo, polo alizidi kumuomba na hatimaye mwenzake akamwachia nafasi kwa masharti makali.

Mkimaliza mchezo wenu unifulie shuka kuondoa uchafu wenu. Na iwe mara ya mwisho, usinizoee,” jamaa alimwambia polo.

Polo alichukua ufunguo na kuenda kasi kumleta msichana akate kiu yake.

Hata hivyo, mambo yalienda kombo kitanda kilipovunjika muda mfupi baada ya polo na binti kuanza kupandishana mzuka.

“Polo alitueleza kuwa hakutaka tatizo hilo kumharibia raha bali alihamisha mchuano kwenye sakafu na wakapiga hatua vizuri,” mdaku alituarifu.

Baada ya muda mrefu walitoka wakiwa na uchovu tele na njiani wakampata mwenye chumba akielekea kwake.

“Polo alimshukuru kwa ukarimu wake kisha akamwarifu kuhusu kuvunjika kwa kitanda,” mdaku alieleza.

Jamaa alilipuka kwa hamaki na kumtaka polo amnunulie kitanda kipya haraka.

Polo hakuwa na lingine ila kuelekea kwa fundi na kununua kitanda kisha akampelekea jamaa kabla ya kuenda zake akikadiria hasara kwa kutamani ufuska.