Kimataifa

'Aliyefanya ngono' na BMW ajitetea kortini ilikuwa presha ya kazi

February 7th, 2019 1 min read

MASHIRIKA Na PETER MBURU

MMILIKI wa baa moja nchini Uingereza aliwapa filamu ya bure wakazi wa Jijini London wakati alivua nguo zote na kusalia uchi wa mnyama, kisha akaanza ‘kufanya ngono’ na gari lake, lakini akaishia mahakamani kujibu mashtaka.

Bw Michael Jameson, mwanamume wa miaka 37 alitoka ndani ya gari lake aina ya BMW kupitia dirisha, kisha akaanza kupanda gurudumu la gari kwa kuchezacheza.

Mfanya biashara huyo alikamatwa na polisi, huku kanda ya video ambayo upande wa mashtaka ulitoa kortini ikionyesha jamaa huyo akiwa uchi chini ya gari.

Shahidi mmoja alieleza korti kuwa alimwona mwanamume huyo akiwa amelalia sehemu ya mbele ya gari akiwa uchi.

Wakili wake Patrick Geddes alieleza korti kuwa ijapokuwa kisa hicho hakikuwa cha kawaida, mteja wake alikuwa amejutia matendo yake na aliomba msamaha.

“Bw Jameson hata ameshindwa kueleza vitendo vyake, alikuwa ameathiriwa na presha nyingi ya kazi. Anaonekana kama aliyekuwa amepoteza fahamu. Ameshtuka na kuaibika sana,” akasema wakili huyo.

Kisa hicho kilitokea mnamo Juni mwaka uliopita.

Alipigwa marufuku kuendesha gari kwa mwaka mmoja, akaamrishwa kuhudhuria matibabu ya akili na afanye kazi bila kulipwa kwa saa 80.

“Kisa hicho cha kukiuka maadili mbele ya umma kilikuwa cha kushangaza na wewe ama sisi hatuwezi kukielezea,” akasema mwenyekiti wa korti Joanna Lindfield.

Kisa hicho kilitokea baada ya kingine mnamo 2015, ambapo Paul Bennett, jamaa mwingine wa miaka 45 alipatikana akifanya ngono na boksi la barua eneo la Wigan.