NA PHILIP MUYANGA
MAHAKAMA ya rufaa imefuta hukumu ya kifungo cha miaka 28 ambayo mwanamume aliyeshtakiwa kwa mauaji ya jamaa yake kwa kisingizio cha uchawi, alipewa.
Majaji Gatembu Kairu, Pauline Nyamweya na Jessie Lesiit walisema Bw Kahindi Mwasambu Kai, aliwasilisha ushahidi wa kutosha kujitetea kwamba ushahidi uliotumiwa kumhukumu haukufikia viwango vilivyostahili kisheria.
Bw Kai alikuwa ameshtakiwa kwa mauaji ya Harrison Tinga, yaliyotokea Septemba 20, 2016 kijijini Matsangoni Kona Mbaya, Kaunti ya Kilifi.