Habari Mseto

Aliyekuwa mbunge wa Belgut afariki

October 18th, 2020 1 min read

NA VITALIS KIMUTAI

Aliyekuwa mbunge wa Belgut  Welsey Kimngeno Rono alifariki Jumamosi baada ya kugojeka kwa muda mfupi. Mwanawe alisema Brian Rono alifariki akiwa hospitali ya Siloam mji wa Kericho.

“Aligonjeka na akapelekwa Siloam ambapo alifariki baada ya kulazwa hospitalini kwa siku mbili,” alisema.

Alisema kwamba mwili wake ulipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti  cha hospitali hiyo na mazishi yake yatafanyika Oktoba 24 nyumbani kwake Masarian eneobunge la Belgut.

Mbunge huyo aliacha watoto wanane. Kabla ya kuwa mbunge alikuwa mwalimu mkuu wa Shule ya Upili ya Cheptenye.

Gavana wa Kericho Paul Chepkwony alimtaja Bw Rono kuwa kiongozi wa heshima.

“Tunaomba mungu aipe familia yake amani. Rono ameenda kuwa malaika akiwa na umri wa miaka 95. Tunashukuru kwa huduma aliyotoa kwa eneobunge hili wakati wake,” alisema.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA