Habari Mseto

Aliyelemewa kulipa benki mkopo aokolewa na korti

August 13th, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Ni afueni kwa mkazi mmoja wa Nairobi baada ya mahakama kutoa agizo la kuzuia kufukuzwa kwake nyumbani na mkopeshaji.

Benki ya Cooperative ililenga kunadi nyumba ya Mzee Eric Muchina Kimani kupata pesa za mkopo iliyotoa kwake.

Agizo la kusimamisha mnada huo lilitolewa na Jaji Grace Nzioka katika Mahakama Kuu, ambapo hatua hiyo imesimamishwa hadi kesi kuhusu mkopo wa Sh53 milioni itakapoamuliwa.

Mnada huo ulitarajiwa kufanyika Jumatano Tassia.

Jaji huyo alimwagiza wakili wa Mzee Muchina, Bw Titus Koceyo kuwasilisha nakala ya maagizo ya mahakama kwa Benki ya Cooperative na John Ngunjiri Mwangi (Ebenezer Autospares & Motorcycles).

Bw Muchina alikuwa amemdhamini Bw Mwangi mkopo wa Sh12 milioni lakini miezi sita baadaye, aliletewa bili ya Sh34, 266,371.