Kimataifa

Aliyembaka mja mzito auawa

May 15th, 2019 1 min read

MASHIRIKA Na PETER MBURU
 
DURBAN, Afrika Kusini
 
MUME aliyempata mwanamume akimbaka mkewe mja mzito nchini Afrika Kusini alimkata kwa panga na kumuua, kaskazini mwa taifa hilo jijini Durban.
 
Kisa hicho kilitokea Jumatatu saa tano asubuhi, wakati mbakaji huyo alivunja na kuingia nyumbani kwa wanandoa hao mume akiwa nyumbani, lakini katika chumba tofauti na akaanza kumdhulumu kingono mkewe.
 
Waokoaji walisema mwanamume aliyekuwa amejihami na panga refu alijaribu kumbaka mwanamke huyo aliyekuwa na uja uzito wa miezi mitano.
 
Hata hivyo, mayowe ya mwanamke huyo yalisikika na mumewe ambaye alikuwa katika chumba kingine cha kulala na akakimbia kumuokoa.
 
Mume alimnyanganya panga yake mbakaji na akamkata nayo kichwani na kwenye mikono, shirika la Times Live likaripoti. Mwanamume huyo alidaiwa kuvuja damu hadi kufa.
 
Baadae polisi waliwasili na kumkamata mumewe mwanamke huyo, huku wakianzisha uchunguzi kuhusu kisa hicho.