Habari Mseto

Aliyemuua mjombake auawa na wakazi

October 26th, 2020 1 min read

NA FAUSTINE NGILA

Mwanamume wa miaka 23 alivamiwa na kuuawa papo kwa hapo na wanakijiji waliojawa na ghadhabu na kujeruhiwa vibaya kwa kumuua mjomba wake katika Kijiji cha Cherangany Kaunti Ndogo ya Trans Nzoia.

Julius Wanduli Membo anayesemekana kuwa mlevi alimuua mjombake Patrick Simiyuwa mika 52 Jumanne nyumbani kwake kwenye kinachpaminika kuwa kilikuwa mzozo wa kinyumbani.

Wanduli alienda nyumbani kwa mjombake eneo la Matisi kumtafuta mamayke baada ya kutororka nyumbani kwake baada ya mzozo kati yao wawili Jumatatu usiku.

Bw Wanduli alianza vita na fundi wa umeme aliyekuwa ametembelea boma hilo huku ikimlazimu mjoambake aingililie kati

Tulikuwa kwa nyumba tukiangalia televisheni wakati binamu yangu alimvamia fundi huyo huku akitaka kujua majina yake na nini kilichomleta hapo.Hap ndipo babayangu alilazimika kuingililia kati kuwatrnganisha ,”alisema Ann Nabangala mwananwe mwendazake .

Bw Simiyu alijsribu kuwatenganisha lakini juhudi zake zikazua baalaa kwani Wandui alimgoga kichwani kwa kutumia jembe jambo lililoshangaza familia hiyo.

“Nilipokimbia chumbani nilipata bwana yangu akiwa amelala ndani ya damu.Nilipiga duru huku majirani wakaja na kumvamia Wanduli na masilaha za aina nyingi hadi wakamuua,”alisema bibi ys Bw Simiyu Violet Nekesa.

Nilipofika hapo nilipata miili miwili ikiwa imelala chini na nikajulisha maafisa wa polisi,”alisema mmoja wa wanakijiji.