Habari Mseto

Aliyemuua polisi Parklands aingia mitini

November 18th, 2020 1 min read

NA FAUSTINE NGILA

Afisa wa polisi anayeaminika kuwa kuhudumu kwenye kituo cha polisi cha Parklands, Nairobi alipigwa hadi kifo na mfanyabiashara mmoja kwenye soko la Ngara Nyayo.

Kisa hicho kiliripotiwa kwenye kituo cha polisi cha Pangani nambari ya OB 76/17/11/2020 saa kumi na dakika arobaini na nane.

Walioshuhudia walisema kwamba afisa huyo alikuwa anazozana na mshukiwa Willy amaafuru kama Rasta kuhusiana na simu iliyosemekana kuwa kuukuu kwenye duka lake.

Mzozo ulizidi na hapo ndipo mfanyabiashara huyo alimgonga afisa huyo akaanguka huku wakisema kwamba mshukiwa pia alimkanyanga afisa huyo tumboni huku akimuua.

Mshukiwa huyo alitoroka kutoka  eneo la tukio baada ya kufanya kitendo hicho.

Maafisa wa polisi kutoka Pangani walitembelea eneo hilo kabla ya kupeleka mwili huo kwenye hospitali ya Chuo Kikuu cha Kenyatta. Mshukiwa huyo bado ako mafichoni, polisi walisema.