Habari Mseto

Aliyenaswa na CCTV akiiba kwenye gari akamatwa

September 28th, 2020 1 min read

NA FAUSTINE NGILA

Maafisa wa upelelezi Mombasa walikamata mwanaume anayeaminika kuwa kati ya washukiwa wa wezi wawili walionaswa kwenye kamera ya CCTV wakiiba kwenye gari maeneo ya Nyali.

Mshukiwa huyo Boris Mutua Malai alikamatwa nyumbani kwake Kiembeni kwenye operesheni iliogozwa na mkuu wa DCI Antony Muriithi..

Gari aina ya Toyota Ractis lililotumika na majambazi hao kuhepa baada ya kutekekeleza wizi nje ya jingo la Texas lilikamatwa  pia.

Kulingana na video hiyo ya CCTV ambayo ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii gari lenye usajili KCP 113P ndilo lilitumika kutekeleza wizi. Lakini DCI ilisema waliopata lilikuwa na nambari ya usajili KCX 726Q.

“Kulingana na ujumbe kutoka kwa jamii timu ya wapelelezi wakiogozwa CCIO walikamata Mutua Malai nyumbani kwake Kiembeni na kukamata gari aina ya Toyota Ractis lenye usajili KCX726Q,”alisema DCI kwenye ujumbe aliouandika kwnye mtandao wa Twitter.

Ujumbe huo uliongeza kwamba polisi wanaendelea kutafuta wazake Bw Mutua waliohusika kwenye wizi huo..

Kwenye video hiyo mwanaume anayeaminika kuwa Bw Mutua na mwezake wanaonekana kuiba kwenye gari lenye rangi nyeupe lililokuwa limeegeshwa tukio lillotokea Alhamisi wiki iliyopita.

Wanaaminika kubadilisha nambari ya usajili ya  gari walipotekeleza wizi huo.