Habari Mseto

Aliyeshtakiwa kuua ataka mahakama imhukumu upesi

February 23rd, 2024 1 min read

NA BRIAN OCHARO

MSHUKIWA wa mauaji Robert Kinisu Waliaula ambaye amegonga vichwa vya habari kwa tuhuma za mauaji ya ajabu ya wanawake wawili, ameiomba mahakama kumpa tarehe ya hukumu.

Bw Waliaula alitoa ombi hilo baada ya wakili wake kukosa kuwasilisha stakabadhi zake za mwisho mara kadhaa licha ya kupewa muda na mahakama kufanya hivyo.

“Wakili wangu ameomba nyongeza ya siku saba ili kuwasilisha stakabadhi hizo lakini inaonekana ana tatizo. Hata nilipofanya maombi ya dhamana, hakuwasilisha stakabadhi hizo. Kama hatakuwa amefanya hivyo wakati kesi hii itakapotajwa tena naiomba mahakama hii ifanye uamuzi wake,” alisema Waliaula.

Bw Waliaula ana kesi ya kujibu kuhusu mauaji ya mfanyabiashara wa Mtwapa Jacqueline Ngina Kitheka na kuficha mwili wake kwenye kabati la nguo.

Mwanamke huyo aliuawa kati ya Mei 3 na Mei 6, 2021, nyumbani kwake Mtwapa.

Kesi hiyo itatajwa Februari 29, 2024.