Habari Mseto

Aliyetabiri atafariki Agosti aangamia kwa corona

August 24th, 2020 1 min read

NA CHARLES WANYORO

Afisa wa ukaguzi wa KEBS aliyetabiri kifo chake  mwaka jana kwamba angefariki mwezi Agosti alifariki kutokana na ugonjwa wa virusi vya corona.

Juma Kaiburi Baitairi (Abdulmalik) alifariki Agosti 18 siku ambayo angefikisha miaka 32 na kuzikwa Agosti 21 kijijini  Antuanthenge, Kaunti ya Meru.

Agosti 1,2019 aliandika kwenye mtandao wa kijamii: “Agosti ni ya thamana kwangu sana kwani ndio mwezi  nilizaliwa, nikatahiriwa, ndio mwezi nilijiunga na chou kikuu na labda ndio mwezi nitafariki nani anajua? Ubarikiwe mwezi wa mfalme.”

Rafikiye Kaiburi Jurgen  Murungi, ambaye ndiye alikuwa mwenye sherehe alisema kwamba tahadhari hiyo iliwashangaza wengi.

“Hata Sheikh aliyeendesha shehere hiyo ya mazishi alitaja jambo hilo. Ilikuwa ni unabii lakini hakuna mtu alichukulia kwa uzito maneno hayo hadi yalipotimia”

Bw Kaiburia alikuwa mtu aliyewachangamsha wafuasi wake kwenye mitandao ya kijamii na alikuwa  anauonea fahari utamaduni wa Meru. Alitajwa kuwa mwenye bidii, mchangamfu, mcheshi na mwangalifu.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA