Habari Mseto

Aliyetaka kuuza mayai wawili kwa Sh600,000 abambwa

October 7th, 2020 1 min read

NA FAUSTINE NGILA

Mwanamume aliyetajwa kuendeleza ulaghai na polisi amekamatwa na maafisa wa DCI  alipokuwa kwenye shughuli za  kuuza mayai mawili kwa Sh600,000.

Mwanamume  huyo aliyetambulika kama Joseph Gakono alikamtwa baada ya wakazi kujulisha polisi kumhusu baada ya malalamishi kuenea Gichugu, Kaunti ya Kirinyanya.

Akithibitisha kukamatwa kwa mwanaume huyo kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Gichungu Antony Mbogo alisema kwamba wapelelezi walimnasa kwa kuchukua pesa kutoka kwa wananchi kwa kutumia njia za udanganyifu.

“Mshukiwa huyo amekuwa mafichoni baada ya kupata Habari kwamba polisi walikuwa wanamtafuta.Alikuwa pia anatishia kuwaua waathiriwa baada ya kuomba warudishiwe pesa zao,’alisema Bw Mbogo.

Mapema mwaka huu mshukiwa huyo anaamikina kuchukua pesa kiasi cha 98,000 kutoka kwa Bi Caroline Karimi huku akimdanganya kwamba angemuuzia kuni.

Kwenye kisa kingine alisemekana kuchukua kiasi cha pesa cha 320,000 kutoka kwa Bw Joseph Mwangi baada ya kumdanganya kwamba angemuuzia shamba eneo la Kutus.

Polisi wanaomba kumzuilia zaidi kwa siku mbili aidi kabla ya kufikishwa kortini ili aandikishe taarifa.