Aliyetekwa arudi nyumbani baada ya miezi mitano

Aliyetekwa arudi nyumbani baada ya miezi mitano

NA KALUME KAZUNGU

Mwanamume wa miaka 39, Taimur Kariuki Hussein, ambaye alitoweka katika hali tatanishi karibu miezi mitano iliyopita hatimaye amepatikana.

Bw Taimur, ambaye ni mkazi wa Watamu, Kaunti ya Kilifi, aliripotiwa kutoweka siku chache baada ya kutiwa nguvuni na maafisa wa polisi wa kukabiliana na ugaidi (ATPU) wakati akielekea Lamu.Akithibitisha ripoti hiyo, mama yake, Bi Zeinab Hussein,71, alisema mwanawe alirudi nyumbani Jumamosi saa tatu asubuhi akiwa hali shwari kiafya.

Bw Taimur alikamatwa Juni 11 wakati akiwa safarini kuelekea Lamu na kuachiliwa bila ya familia kukabidhiwa jamaa wao mikononi. Bw Taimur ni mzawa wa pili katika familia ya watoto watatu. Katika mahojiano na Taifa Jumapili, Bi Hussein hakuficha furaha yake kufuatia kurudi nyumbani kwa kijana wake.

“Nina furaha tele. Mtoto wangu amerudi nyumbani leo asubuhi, akiwa hali shwari. Kwa sasa tumemwacha apumzike kwanza. Mola amejibu maombi yangu ya muda mrefu kwamba mwanangu arudi nyumbani akiwa hai,” akasema.Ndugu mkubwa wa Taimur, Ahmed Wanyee Kinuthia pia hakuficha furaha yake kufuatia kurudi nyumbani kwa kaka yake.

Bw Kinuthia alisema zaidi ya miezi mitano ya kutoweka kwa nduguye, ilikuwa kama jehanamu kwa familia yao.Kulingana na Bw Kinuthia, kakaye mdogo ni mpenda amani na asiyejihusisha na vitendo vyovyote vya uhalifu na kuwa kupotea kwake ni jambo lililokuwa likiwakosesha usingizi kama wanafamilia.

“Hata kula na kulala ilikuwa shida kila tulipokuwa tukifikiria kuhusu hali ya ndugu yetu Taimur kokote alikokuwa. Leo tuna furaha kuu kuwa hatimaye amerudi nyumbani akiwa hai. Tunamshukuru Mungu,” akasema Bw Kinuthia.Naye dada yake mdogo, Fauziya Hussein alishukuru kila sekta, wakiwemo wanahabari kwa kuangazia na kushinikiza kupatikana kwa nduguye.

Bi Fauziya alisena ombi lake pia ni kwa familia nyingine zilizopoteza wapendwa wao katika hali tatanishi pia warudi nyumbani wakiwa hai kama alivyorudi nduguye, Taimur.’Langu tu ni kushukuru Mungu na wote waliotusaidia kusukuma kupatikana kwa ndugu yangu,Taimur,ikiwemo nyinyi wanahabari,’ akasema Bi Fauziya.

Taimur alizaliwa 1982 na kukulia jijini Mombasa kabla ya kujiunga na Shule ya Msingi ya Nairobi.Baadaye alijiunga na shule ya upili ya Upper Hill jijini Nairobi alikojizolea alama ya A- mwaka 2000.Kisha akajiunga na taasisi ya masuala ya teknolojia ya Intel jijini Nairobi.

Mwaka 2004 alienda Marekani kuongeza masomo yake ya Teknolojia na Mawasiliano.Aidha changamoto za kifedha zilimfanya akaacha masomo yake na kurudi Kenya

You can share this post!

JAMVI: Roho ya Uhuru iko kwa OKA au Raila?

Serikali haitaweka vikwazo dhidi ya wageni kuingia Kenya...

T L