Kimataifa

Aliyetishia kuua msichana na kula maiti yake anaswa

November 1st, 2018 1 min read

NA MASHIRIKA

Miami, USA

MWANAMUME alikamatwa na polisi baada ya kutangaza mtandaoni kwamba angependa kuua msichana mwenye umri mdogo kisha afanye ngono na mwili wake na kula maiti yake.

Alexander Barter, 21, alikamatwa baada ya polisi kujifanya baba aliyejitolea kumpa binti yake kwa hiari.

“Kesi hii ni ya kushangaza na kuchukiza zaidi ambayo nimewahi huona,” mkuu wa polisi wa Kaunti ya Brevard iliyo Florida, Wayne Ivey, alisema kwenye kikao cha wanahabari.

Upelelezi ulianzishwa wakati afisa wa polisi wa Brevard alipoona tangazo kwenye intaneti ambapo Barter alisema angependa kujaribu kufanya ngono na maiti kisha ale mwili wa msichana tineja.