Amani: Kalonzo kutuzwa leo Dubai

Amani: Kalonzo kutuzwa leo Dubai

Na CHARLES WASONGA

KIONGOZI wa Wiper Kalonzo Musyoka leo Jumatatu atakuwa miongoni mwa watu watakaopokezwa tuzo mbali mbali Dubai kutokana na ufanisi wao katika nyanja mbalimbali za maisha.

Bw Musyoka ambaye aliwasili Dubai jana Jumapili, atatuzwa kutokana na juhudi zake katika kurejesha amani nchini Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Somalia; kando na ukuzaji demokrasia kwa ujumla.

Atapokezwa tuzo ya ‘The Icon of Democracy Award 2021’ ambayo pia inatambua juhudi za Makamu huyo wa Rais wa zamani katika kubuniwa kwa Serikali ya Muungano Mkuu nchini Kenya mnamo 2008.

Kando na masuala ya uongozi, amani na demokrasia tuzo hiyo kwa jina ‘Voice Achievers Award for 2021’ inayodhaminiwa na jarida la The Voice News Magazine pia hutuza wafanyabiashara ambao huleta mabadiliko bora katika jamii au nchi au maeneo wanakohudumu.

“Pia huwa tunahimiza maendeleo ya kijamii na nchi kwa ujumla. Tunaamini kuwa washindi wa mwaka huu, sawa na mwaka uliopita, watatimiza malengo ya tuzo hii,’’ akasema Pasta Elvis Iruth, ambaye ni mchapishaji wa The Voice News Magazine yenye makao yake nchini Uholanzi.

You can share this post!

Viongozi kukongamana kwa mkutano wa UNGA

Kenya Police warapua Vihiga kuingia FKF-PL