Bambika

Amber Ray na Kennedy Rapudo wathibitisha ladha ya penzi ni mtoto

February 1st, 2024 1 min read

NA FRIDAH OKACHI

SOSHIOLAITI Amber Ray na mpenziwe Kennedy Rapudo almaarufu ‘Tajiri’, kwa mara ya kwanza wameiweka sura ya binti yao Africanah Rapudo kwenye mitandao ya kijamii tangu azaliwe miezi kadha iliyopita.

Kweli ladha ya penzi ni mtoto!

Wawili hao, jinsi wanafahamika kuwa na vitimbi na wanamitandao, waliandaa sherehe nyumbani kwao na kukaribisha marafiki wao kwa ajili ya siku hiyo muhimu kwa binti yao.

Katika sehemu ya nyumba yalipambwa maua ya waridi kwa wingi.

Waliohudhuria walivalia mavazi ya rangi nyeusi, wanaume wakilazimika kuvalia suti na Tuxedo huku wanawake wakivalia mavazi yenye muundo wa kipekee.

Katika video hiyo iliyosambazwa mtandaoni, watu mashuhuri kama vile Oga Obinna ambaye kwa wakati mwingi hujiit  crush wa Amber Ray, sosholaiti Risper Faith, Eric Omondi ni miongoni mwa waliowahi kwenye hafla hiyo ya kipekee.

Video iliyosambazwa na BNN, ilionyesha wageni hao wakiwa wamekusanyika sebuleni, huku wazazi wa mtoto wakionyeshana sura wakiwa kwenye ngazi au stairs za juu.

Pia, walisikika wakifurahia na kumsifia binti huyo.

“Ni mrembo lakini anashangaa hawa ni akina nani. Anashangaa ni akina nani wamejazana katika sehemu hii,” mmojawapo wa waliofika alisikika akisema.

Mtoto huyo alizaliwe Mei 2023.

Wazazi wake walikuwa na mazoea ya kumtaja kwenye video walizokuwa wakichapisha kwenye mitandao kwa kumuita jina bila kuweka sura hiyo wazi.

Wazazi hao wanafahamika kuishi na watoto wao wengine katika nyumba hiyo.

Mwaka 2023 Tajiri aliomba Amber Ray msamaha baada ya kitendo kilichoashiria dhuluma ya kijinsia iliyokuwa imesababisha wawili hao kutengana kwa muda.