Habari Mseto

Amdunga kisu mumewe mara 11 wakizozania kuosha vyombo

June 6th, 2020 1 min read

NA Joseph Wangui

Mwanamke mmoja aliyemuua mpeziwe wakibishana nani atakayeosha vyombo baada ya chakula cha jioni amekatazwa ddhamana baada ya kusoka kuwakilisha maelezo ya mahali akatapokuwa akiishi baada ya kuachiliwa.

Susan Njeri Wachiuri, mwenye umri wa miaka 25 alikuwa anataka aachiliwe kwa dhamana lakini jaji James Wakiaga akasema kwamba hakukuwa na ushaidi wa kutosha kwamba mshukiwa angetoroka.

“Kwa kukosekana maandishi ya ushaidi wa wapi mshukiwa ataishi baada ya kuachilliwa ,isipokuwa kwa nyumba ya marehemu ambapo kitendo cha mauaji kilifanyika hivo nashawishika kuwa itakuwa hatari kuachilia mshukiwa kwa thamana”,alisema jaji Wakiaga.

Ms Wachiuri anashtakiwa kwa kumdunga kisu Kevin Ng’ang’a mara11 tarehe 9 mwezi Aprili 2020 katika mtaa wa White House, Tena Estate, Kaumukunji kaunti la Nairobi.

Alikanusha kuwa kutenda kitendo hicho,.

Huku akiomba kuachiliwa na thamana Bi Wachiuri aliambia korti kwamba alikuwa na familia ya kumsaidia na wako tayari kumpokea.

Huku akikataa kumwachlia kwa dhamana hakimu huyo akisema kwamba vita dhidi ya jinsia vimeongezeka kwahivo mshukiwa anapaswa kunyimwa thamana.