Amref yamtaka Uhuru aondoe kafyu

Amref yamtaka Uhuru aondoe kafyu

Na LEONARD ONYANGO

SHINIKIZO la kumtaka Rais Uhuru Kenyatta kuondoa agizo la watu kutokuwa nje usiku (kafyu) zinaongezeka.Shirika la Amref Health Africa ndilo la hivi karibuni kumtaka Rais Kenyatta kuondoa kafyu likisema kuwa nchi inastahili kufunguliwa.

Badala yake, Mkurugenzi Mtendaji wa Amref Dkt Githinji Gitahi, Jumapili alisema serikali inafaa kuelekeza juhudi zake katika kuhimiza wananchi kujitokeza kuchanjwa.

Dkt Githinji ambaye ni mwanachama wa Jopokazi la Kukabili Ugonjwa wa Covid-19 barani Afrika, alisema kuwa kafyu inaumiza uchumi wa nchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Amref Dkt Githinji Gitahi. Picha/ Hisani

Dkt Githinji, hata hivyo, alikiri kuwa kafyu ilisaidia pakubwa kupunguza maambukizi ya virusi vya corona nchini katika siku za mwanzo.

“Kafyu zilizowekwa na mataifa mbalimbali zilisaidia kupunguza maambukizi ya corona. Hii ni kwa sababu tabia ya binadamu mchana ni tofauti na usiku. Lakini maelfu ya watu wamepoteza kazi kutokana na kafyu na uchumi wa Kenya umedorora. Hivyo, wakati wa kuondoa kafyu umewadia,” akasema Dkt Githinji.

Mkurugenzi Mtendaji wa Amref pia alisema kuwa kafyu imetumiwa vibaya na maafisa wa polisi kutekeleza unyama dhidi ya Wakenya.

Rais Uhuru Kenyatta alitangaza kafyu ya nchi nzima kwa mara ya kwanza mnamo Aprili 2020, na kuanzia wakati huo amekuwa akiongeza muda wayo.

Mnamo Agosti 19, 2021, Rais aliongeza muda wa kafyu ya kuanzia saa nne usiku hadi saa kumi alfajiri kwa siku 60.

Muda huo unatarajiwa kukamilika Oktoba 18, siku mbili kabla ya sherehe za Mashujaa zitakazofanyika katika Kaunti ya Kirinyaga.

Wakenya wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kushinikiza Rais Kenyatta kuondoa kafyu.

Jumapili, wizara ya Afya, ilitangaza vifo tisa hivyo kufikisha jumla ya watu 5,140 ambao wameangamia kutokana na janga la corona.

Watu 91 kati ya 3435 waliopimwa ndani ya saa 24 zilizopita walipatikana na virusi vya corona na kufikisha idadi ya visa nchini 250,114.
Dordogne: she hits her partner with a weight bar buy alphabolin vial methenolone enanthate primobolan depot with uk shipping 4 rules to follow for a successful bodybuilding program conseilmuscu bodybuilding tips.
Wakati huo huo, serikali imetangaza kuwa itaanza kutoa chanjo ya Pfizer kuanzia leo Jumatatu.

You can share this post!

Ruto amlima Uhuru

Mabadiliko yafanyika katika ngazi za utawala maeneo kadha...