Habari Mseto

Amuua mwanawe kisha kujiua

October 20th, 2020 1 min read

NA MACHARIA MWANGI

Mwanamume mmoja amejiua baada ya kumuua mwanawe wa miaka tatu Kijiji cha Moi Ndambi, Kaunti ya Nakuru, Jumanne.

Naibu Chifu wa eneo la Kipkunyo  Simon Koskei alisema kwamba mwanamume  huyo alikuwa ametengana na mkewe kufutia mzozo wa kinyumbani.

Chifu huyo alisema mshukiwa huyo aliatambuliwa kama Daniel Kyallo na alikuwa anapitia maisha magumu baada ya mkewe kumtoroka.

“Waliokuwa karibu naye walisema kwamba alionekana mtu mwenye taabu baada ya mkewe kutoroka nyumbani kwao, wiki moja iliyopita,” alisema Bw Koskei..

Chifu huyo alisema kwamba mwathiriwa huyo kwanza aliua mwanawe na kuweka mwili wake kwenye shimo la choo lililokuwa linajengwa kwa kutumia gazi.

“Alitumia ngazi hiyo kujinyonga Jumanne asubuhi,” alisema chifu huyo.

Miili ya  wawili hao ilipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti cha Naivasha.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA