Habari Mseto

Amuua nduguye mkubwa kwenye wakizozana

October 15th, 2020 1 min read

NA VITALIS KIMUTAI

Mzozo kati ya ndugu wawili Kaunti ya Bomet ulisababisha kifo baada ya mmoja kumdunga mwezake kwa kisu Jumatano usiku.

Bw Geoffrey Siele alidungwa mara kadhaa kifuani na mgongoni na dunguye mdogo Jacob Silele kwenye Kijiji cha Saptet wadi ya Chepchabas eneobunge la Konoin baada ya mzozo ambao haukujulikana.

Kufuatia tukio hilo mwathiriwa alikimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Kericho ambapo alifariki kutokana na majeraha alipokuwa akitibiwa na daktari.

Kamanda wa polisi wa Alex Shikondi alithibitisha kwamba mshukiwa alikamatwa na anazuliliwa kwenye kiyuo cha  polisi cha Mogogosiek.

“Kisu kilichotumiwa kumuua mwathiriwa kilipatiana kwenye eno la tuko lililotokea saa tatu usiku Jumanne,” alisema Bw Shikondi.

BW Richard Rono, chifu wa eneo hilo alisema  ndugu hao wawili walizozana kabla ya mdogo kuchukua kisu na kumdunga mkubwa .

Kumekuwa kukishuhudiwa mauaji kwenye kaunti hiyo, na maujai mengi hutokana na maswala ya mapenzi, pombe na mzozo wa kifamilia.