ANC yafufua wito Mudavadi awe naibu wa Ruto

ANC yafufua wito Mudavadi awe naibu wa Ruto

NA WINNIE ATIENO

WANACHAMA wa Amani National Congress (ANC), wamefufua wito kumtaka Naibu Rais William Ruto, kumchagua kinara wao, Bw Musalia Mudavadi, kuwa mgombea mwenza wa urais.

Wakiongozwa mbunge wa Matuga, Bw Kassim Tandaza, ambaye pia ni naibu kiongozi wa ANC, walisema Bw Mudavadi ana tajriba ya kutosha kuwa naibu rais.

Wakiendelea kumpigia debe Bw Ruto Pwani, walisema wana imani ya kuunda serikali kupitia Kenya Kwanza.

You can share this post!

ODM yajiandaa kumnadi Nassir kutwaa ugavana

Raila atuliza vita vya ndani katika Azimio

T L