Habari Mseto

Anyakwa baada ya kubaka msichana

November 14th, 2020 1 min read

NA GEORGE ODIWUOR

Mwanamume wa miaka 40 amekamatwa baada ya kumbaka msichana wa miaka minne Rachuonyo Kaunti ya Homabay.

Akisaidiwa na maafisa kutoka kituo cha polisi cha Oyugis chifu msaidizi wa Kawino Joel Owenga walikamata mshukiwa huyo anayeaminika kupatikana akifanya kitendo hicho na nyanya ya mwathiriwa.

Mshukiwa alimbaka mwatthiriwa wakati nyanyayake alipokuwa alichota maji ya mvua.Msichana huyo alikuwa ametembelea nyanya yake kwenye Kijiji cha Kong’ondo Jumamosi.

“Mshukiwa na mwathiriwa wote ni wamekuwa wakitembelea nyanya huko  kwa muda .Mshukiwa alimrithi nyanya huyo baada ya kifo cha bwanayake,”aalisema chifu huyo.

Aliripotiwa kwamba alimchukua msichana huyo na akampeleka kwenye chumba cha kulala ambapo anaaminika alimdhulumu msichana huyo.

“Wakazi waliokuwa wamejawa na ghathabu walikuwa tayari kumkabilia mshukiwa huyo,hizo nililazimika kuita polisi ili wamwokoe mshukiwa,afisa huyo alisema kwamba  mshukiwa huyo ambaye alikiri kwamba alifanya kitendo hicho  alilaumu mapepo kwa kumsukuma kufanya kitendo hicho.Atashatkiwa kesho ,”alisema Bw Omwega.