Apewa siku moja kurejesha pesa alizoibia mwajiri

Apewa siku moja kurejesha pesa alizoibia mwajiri

NA JOSEPH NDUNDA

MWANAMUME aliyeibia mwajiri Sh22,682 amepewa hadi leo Ijumaa amrudishie au aende jela.

Dancan Hardson Bala, alipewa siku moja na Mahakama ya Kibera kurejesha pesa hizo, baada ya kukiri kuiba pesa hizo za kampuni ya North Wind Delivery Services Oktoba 2020.

Kampuni hiyo ilikuwa imempa kazi ya kusafirisha bidhaa za wateja katika maeneo tofauti.

Anadaiwa kupokea malipo kutoka kwa wateja kwa bidhaa walizonunua japo hakuzipeleka kwa kampuni.

You can share this post!

Majaji kupewa ulinzi zaidi baada ya shambulio

WIKI YA LUGHA ZA KIAFRIKA: Mikakati ya kukuza matumizi ya...

T L