Habari Mseto

Apigwa hadi kufa kwa kuiba miraa

October 18th, 2020 1 min read

NA CHARLES WANYORO

Familia moja kaunti ya Meru inalilia haki baada ya mwanao wa miaka 16 kuvamiwa na wakazi na kupigwa hadi kifo kwa madai ya kuiba miraa.

Anthony Munene Gitonga, mwanafunzi wa darasa la la saba alifariki siku tatu zilizopita baada ya kupewa kichapo.

Ripoti za upasuaji zilionyesha kwamba kijana huyo alifariki kutokana na majeraha kichwani natumboni..

Video na picha zilionyesha kwamba mwanafunzi huyo akiwa amefungwa kwa kamba shingoni na kuwekwa ndani ya gurudumu. Wavamizi hao walimpiga na kumdhulumu hadi kifo.

Bi Elizabeth Kangai nyanyake kijana huyo alisema Munene alipelekwa hospitalini na baadaye kupelekwa hospitali ya rufaa ya Meru ambapo alifariki.

“Nilishangazwa nawalivyo mwathibu kijana huyo .Walimfunga kwa Kamba na kumchapa .Niliripoti kisa hicho kwa polisi lakini hakuna hatua iliyochukuliwa,”alisema Bi Kangai.

Mjomba wa kijana huyo Harrison Mwenda alisema kwamba familia hiyo ilikuwa inatishiwa na waliomuua kijana huyo kwasababu familia hiyo ilikuwa ya matajiri.

“Wanatutishia huku wakisema kwamba hakuna hatua itachukuliwa dhidi yao.Tunaomba serikali itusaindie kupata haki,”alisema. justice to help us,” he said.

Bw  Mwenda alikana kwamba kijana huyo aliiba miraa huku akiongeza kwamba hata kama aliiba angepelekwa polisi. “Alikuwa kijana mdogo ambaye angebandilisha tabia zake kama madai hayo yalikuwa ya kweli,” alisema.

Upasuaji uliofanywa Alhamisi  mbele ya familia na polisi wawili kutoka kituo cha polisi cha Maua uionyesha kwamba kijana huyo alifariki kutokana na maumivu aliyoyapata.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA