Habari Mseto

Aponyoka kunyongwa kumuua mpenzi

December 10th, 2018 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

KIBARUA aliyeshtakiwa kwa mauaji ya mpenziwe Jumatano aliponyoka kitanzi baada ya Mahakama kuu kutupilia mbali kesi dhidi yake.

Hata hivyo Jaji Roselyn Korir alimweleza n Victor Bosire Nyamaya ameachiliwa na sheria  lakini sio eti “ kwamba hakutenda uhalifu.”

Bosire alishtakiwa kwa kumuua Ruth Wanjiku Mwangi mnamo Septemba 16 2010 katika mtaa wa Kawangware Nairiobi.

Jaji Korir alisema kati ya mashahidi tisa walioitwa na upande wa mashtaka hakuna mmoja alishuhudia mauaji hayo ila mshtakiwa alidaiwa ndiye alikuwa mtu wa mwisho kuonekana na mshtakiwa.

Mwili wa Wanjiku ulikutwa nyumbani kwake siku tatu baada ya kuuawa.

Mahakama ilifahamishwa kuwa mwili huo ulikuwa na majeraha ya kudungwa na kisu shingoni , kwenya mapaja na kwenye tumbo.

“Marehemu alionekana akitoka kwenye kilabu cha kuuza pombe akiwa na mshtakiwa,” Jaji Korir alisema.

Mahakama ilimwachilia mshtakiwa lakini ikasema , “hakuachiliwa kwa vile hakuuua mbali ni sheria imewamchilia kwa kukosekana ushahidi wa kumuhusisha moja kwa moja na ushahidi.”