Arati akana dai la kuzua fujo kanisani

Arati akana dai la kuzua fujo kanisani

Na WYCLIFFE NYABERI

Mbunge wa Dagoretti Kaskazini, Simba Arati, amejitenga na madai ya kuzua fujo katika hafla ya kanisa Katoliki, Kaunti ya Kisii.

Bw Arati amesema tukio lililojiri kanisani Nyamagwa, ambapo anasemekana kung’ang’ania kuhutubu ni mbinu ya wapinzani wake kuhujumu azma yake ya kuwa gavana wa pili wa Kisii.Tukio hilo lilipelekea uongozi wa kanisa Katoliki hilo dayosisi ya Kisii kumrejeshea Bw Arati mchango aliotoa wa Sh 100, 000.

‘Kuliko kuzunguka kueneza propaganda, leteni ajenda zenu. Wacheni kuzunguka na kueneza uvumi ambao hauna msingi kuwa nilikosa heshima kanisani,’ Bw Arati akasema katika hafla moja eneo la Metembe, Nyaribari Masaba wakati wa kufariji familia moja iliyofiwa na mpendwa wao.

Akiwa ameandamana na mbunge wa Kitutu Chache Kusini, Richard Onyonka, Bw Arati alidai kwamba wapinzani wake wameingiza baridi kutokana na ujio wake katika siasa za Kisii.Alijipigia debe kwa kusema analenga kuboresha maisha ya wakazi wa Kisii.

You can share this post!

Biden, Putin kujadiliana taharuki ya Marekani, urusi kuhusu...

Washirika wa Ruto wadai Obado avuruga chama cha Naibu Rais

T L